Mazingira FM
Mazingira FM
6 October 2025, 6:38 pm

Wananchi wanapaswa kuwa na utamaduni wa kutafuta ushauri kutoka kwa wataalamu wa sheria, wakiwemo mawakili.
Na Adelinus Banenwa.
Wananchi wameaswa kuacha tabia ya kufuata mikumbo katika kufanya maamuzi, kwani baadhi ya mambo yanayofanywa kwa mazoea au kwa ushawishi wa watu wengine yanaweza kuwasababishia matatizo ya kisheria bila wao kutarajia.
Wito huo umetolewa na Wakili Msomi Kabengwe Matiasi Kabengwe, ambaye pia ni Mrakibu wa Polisi Mkoa wa Mara, wakati akizungumza katika kipindi cha Ufahamu wa Sheria kinachorushwa na Radio Mazingira FM.
Wakili Kabengwe amesema wananchi wanapaswa kuwa na utamaduni wa kutafuta ushauri kutoka kwa wataalamu wa sheria, wakiwemo mawakili, ili kupata ufafanuzi wa kisheria pale wanapokumbana na changamoto mbalimbali katika jamii.

Aidha, amesema kuwa kupitia Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kumekuwa na utaratibu wa kutoa msaada wa kisheria bure kwa watu wasiokuwa na uwezo wa kugharamia huduma za mawakili, hususan kwenye kesi kubwa kama zile za mauaji.
Wakili huyo amehitimisha kwa kusisitiza kuwa elimu ya kisheria ni muhimu kwa kila mwananchi, kwani inasaidia kujenga jamii inayofuata sheria, haki na utulivu.