Mazingira FM
Mazingira FM
6 October 2025, 12:48 pm

Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Twende kutalii Bw.Albert Chenza, amesema kutokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi ,idadi ya watalii wanaotembelea baadhi ya hifadhi inaweza kupungua.
Na Catherine Msafiri
Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Twende kutalii Bw.Albert Chenza, amesema kuwa mabadiliko ya tabia nchi yanaendelea kuwa tishio kubwa kwa sekta ya utalii nchini Tanzania, hasa katika mbuga za wanyama ambazo ni kivutio kikuu cha watalii kutoka ndani na nje ya nchi.
Akizungumza kwenye kipindi cha uhifadhi na utalii kupitia Mazingira FM, Bw. Chenza amesema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kuleta athari kubwa katika mazingira ya mbuga jambo litakaloathiri upatikanaji wa maji, chakula na makazi ya wanyama.
Ameongeza kuwa kutokana na hali hiyo, idadi ya watalii wanaotembelea baadhi ya hifadhi inaweza kupungua, kwani wanyama wataonekana kwa shida, na hivyo kuathiri mapato ya kampuni za utalii pamoja na serikali.
Amebainisha kuwa sababu zinazochangia kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabia nchi ni uzalishaji wa hewa ukaa.Huku akitoa wito kuhama kwenye matumizi yanayochangia kuzalisha hewa ukaa kama matumizi ya kuni na mkaa.