Mazingira FM
Mazingira FM
3 October 2025, 2:51 pm

Getere ameahidi baada ya uchaguzi watatoa million 20 kwaajili ya kujenga mabafu na tenki la maji Esperanto sekondari.
Na Catherine Msafiri
Mgombea ubunge wa jimbo la Bunda Boniface Mwita Getere amewaahidi wanafunzi na uongozi wa shule ya sekondari Esperanto kushirikiana na mgombea udiwani kata ya Ketare pindi watakapoapishwa mara baada ya uchaguzi mkuu wa 2025 wataleta million 20 kwaajili ya kujenga mabafu na matenki ya maji shuleni hapo.
Getere ameyasema hayo alipofika kwenye mahafali ya kidato cha nne katika shule sekondari Esperanto ambapo ametoa pongezi kwa aliyekuwa diwani na ambaye ni mgombea udiwani wa kata ya Ketare kupitia chama cha Mapinduzi CCM Mramba Simba Nyamkinda.
Aidha mgombea ubunge huyo ameahidi watakapomaliza uchaguzi mkuu mwaka huu atatoa shilingi 10000 kwa kila mwanafunzi anayefanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne katika shule hiyo huku akiwataka watulie wafanye vizuri mtihani.