Mazingira FM

Mramba akabidhi sola sekondari ya Esperanto

3 October 2025, 2:10 pm

Mwenyekiti wa shirika la Mazingira na mlezi wa shule ya esperanto sekondari Simba Mramba Nyamkinda akikabidhi sola mbili katika shule ya sekondari Esperanto,picha na Joseph Makori

Mgombea wa udiwani kata ya Ketare Simba Mramba Nyamkinda amekabidhi sola mbili katika shule ya sekondari Esperanto.

Na Catherine Msafiri,

Mwenyekiti wa shirika la Mazingira na mlezi wa shule ya esperanto sekondari Simba Mramba Nyamkinda amekabidhi sola mbili katika shule ya sekondari Esperanto kwaajili ya kusaidia nishati ya mwanga kwenye bweni na bwalo la chakula pindi umeme unapokata.

Mramba amekabidhi sola hizo alipokuwa akizungumza na wanafunzi na wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Esperanto ambapo yeye ndie alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo lakini pia ni mlezi wa shule hiyo.

Sauti ya Mgombea wa udiwani kata ya Ketare Simba Mramba Nyamkinda

Aidha ameahidi kuendelea kusaidia shule hiyo huku akitaja Shirika lake la Mazingira community development forum linampango wa kujenga nyumba za watumishi shuleni hapo.

Sauti ya Mgombea wa udiwani kata ya Ketare Simba Mramba Nyamkinda