Mazingira FM

MCDF wakabidhi chumba cha tehama Esperanto

3 October 2025, 1:47 pm

Wanafunzi wa shule ya sekondari Esperanto wakiwa kwenye chumba cha Tehama, picha na Joseph Makori

Mratibu wa miradi Simba Mramba ameeleza baadhi ya mambo waliyofanya kama shirika katika shule hiyo huku akitaja kuwa chumba hicho kimewekewa viti 31 na meza 31 na computer 30.

Na Catherine Msafiri,

Shirika la Mazingira Community Development Forum limezindua mradi wa chumba maalum cha tehama shule ya sekondari Esperanto uliogharimu shilingi milioni 35 kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi kujifunza masomo ya tehama .

Akisoma risala ya shirika mbele ya mgeni rasmi mratibu wa miradi Simba Mramba ameeleza baadhi ya mambo waliyofanya kama shirika katika shule hiyo huku akitaja kuwa chumba hicho kimewekewa viti 31 na meza 31 na computer 30.

Sauti ya mratibu wa miradi Simba Mramba
Mratibu wa miradi Simba Mramba akiwa kwenye chumba cha Tehama,picha na Joseph Makori

Aidha amebainisha kuwa shirika liko kwenye hatua ya mazungumzo na wadau mbalimbali kutoka maifa mengine ili kusaidia kufadhili mradi wa nishati mbadala utakao saidia wanafunzi na waalimu katika kuendeleza utunzaji wa mazingira kwa kuepuka kukata miti kwaajili ya kupikiaAmeongeza kuwa shirika linaomba hakikisho ya gharama ya kujaza gesi kila mwezi .

Sauti ya mratibu wa miradi Simba Mramba

George s. Mbilinyi Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Bunda aliyekuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi huo ametoa pongezi kwa shirika la mazingira kwa jitihada zao katika kusaidia kwenye sekta mbalimbali
Mbilinyi ametoa maagizo kwa viongozi kuhakikisha wanashirikisha wananchi katika miradi wanayoianzisha na inayosimamiwa na wadau ,kuipa kipaumbele miradi inayoekelezwa na serikali

Sauti ya George s. Mbilinyi Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Bunda

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wameishukuru shirika la Mazingira kwa kuwaletea vifaa na kujenga jengo kwaajiri ya masomo ya tehama
Naye mwalimu wa somo hilo ameeleza namna somo hilo litakavyowasaidia watoto watakapohitimu kwenda kuendana na mabadiliko ya teknolojia.

Sauti za wanafunzi na mwalimu

Mradi huo umefanywa na ushirikiano wa Shirika la Mazingira na STICHTING MAZINGIRA NEDERLAND na WILDE GANZEN FOUNDATION