Mazingira FM
Mazingira FM
3 October 2025, 1:39 pm

Mgombea urais kupitia DP Abdul Juma Mluya aahidi serikali ya DP itarekebisha mtaala wa elimu ili kuendana na teknolojia ya sasa.
Na Teddy Thomas
Chama cha Democratic Paty DP kimesema endapo kitapa ridhaa ya kuiongoza serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu October 29 mwaka huu kitatoa huduma bure kwa mama mjamzito na wakati wa kujifungua.
Hayo yamesemwa na mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya DP Abdul Juma Mluya kwenye kapeni za kusaka kura eneo la Stand ya zamani wilayani Bunda.
Amesema kuwa kitendo cha serikali ya sasa kudai pesa wajawazito wanapokwenda kujifungua ni udhalili hivyo serikali ya DP itawahudumia bure wajawazito hao.
Aidha amesema kuwa serikali ya DP itahakikisha inarekebisha mtaala wa elimu ili kuendana na teknolojia ya sasa.
Pia Mluya amesema chama cha DP kitahakikisha kina boresha maslahi ya watumishi wa umma ili kuendana na hali halisi ya maisha.
Hata hivyo amewaomba wananchi kufanya maamuzi sahihi katika upigaji wa kura ili kuwasaidia na wale wasiojiweza kupata viongozi bora.