Mazingira FM

Rorya kinara wagonjwa wa selimundu Mara

30 September 2025, 1:28 pm

Mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza Bi.Ester Muya na Daktari wa idara ya magonjwa ya watoto Dr.Xavery Njalale wakiwa studio za Radio Mazingira FM,picha na Catherine Msafiri

Halmashauri ya wilaya ya Rorya kinara tatizo la ugonjwa wa selimundu (Sickle cell) kwa asilimia kubwa ikiwa na wagonjwa 1500 kati ya wagonjwa 5037 kwa mkoa wa Mara.

Na Catherine Msafiri

Imeelezwa kuwa Halmashauri ya wilaya ya Rorya ndio kinara ya tatizo la ugonjwa wa seli mundu (Sicle cell) kwa asilimia kubwa ikiwa na wagonjwa 1500 kati ya wagonjwa 5037 kwa mkoa mzima. Hayo yamebainishwa na mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza kutoka ofisi ya mganga mkuu mkoa wa Mara Bi. Ester Muya wakati akitoa elimu kuhusu tatizo la seli mundu kupitia kipindi cha kapu letu.

Aidha amebainisha kuwa wapo watu wanaoamini kuwa ni tatizo la seli mundu ni la kulogwa

Sauti ya mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza kutoka ofisi ya mganga mkuu mkoa wa Mara Bi.Ester Muy

Kwa upande wake daktari wa idara ya magonjwa ya watoto kutoka Hospitali ya Rufaa ya mwalimu Nyerere Dr.Xavery Njalale amesema tatizo la seli mundu ni la kurithi kutokana na wazazi wote wawili kuwa na vinasaba vya tatizo hilo

Ameongeza kwa kubainisha dalili za tatizo la seli mundu ikiwa ni pamoja na kuvimba miguu na vidole,manjano kali na maumivu ya mwili

Sauti ya Daktari wa idara ya magonjwa ya watoto kutoka Hospitali ya Rufaa ya mwalimu Nyerere Dr.Xavery Njalale
Mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza Bi.Ester Muya na Daktari wa idara ya magonjwa ya watoto Dr.Xavery Njalale wakiwa studio za Radio Mazingira FM,picha na Catherine Msafiri

Dr.Xavery Njalale amesema kuwa yapo madhara ya yanayowezakumpata mtu mwenye tatizo la seli mundu kwa haraka na baada ya muda,kama kiharusi na kuishiwa damu mara kwa mara

Sauti ya Daktari wa idara ya magonjwa ya watoto kutoka Hospitali ya Rufaa ya mwalimu Nyerere Dr.Xavery Njalale

Hata hivyo Dr.Xavery Njalale amebainisha kuwa kuna makundi matatu ya matibabu ya seli mundu

Sauti ya Daktari wa idara ya magonjwa ya watoto kutoka Hospitali ya Rufaa ya mwalimu Nyerere Dr.Xavery Njalale