Mazingira FM
Mazingira FM
30 September 2025, 12:12 pm

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) yasema wanaomiliki nyara kama pembe, na mikia ya wanyamapori bila vibali , ni kinyume na sheria za uhifadhi .
Na Catherine Msafiri,
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imewataka wananchi kuhakikisha wanamiliki nyara za serikali kwa kufuata sheria.
Akizungumza kwenye kipindi cha uhifadhi na utalii kinachoruka radio Mazingira FM, Awena Salum ambaye ni Afisa utalii kutoka TAWA kanda ya ziwa amebainisha kuwa kumekuwa na watu wanaomiliki nyara kama pembe, na mikia ya wanyamapori bila vibali , jambo ambalo ni kinyume na sheria za uhifadhi.
Afisa huyo wa TAWA ametoa wito kwa wananchi wote wanaomiliki nyara za serikali kinyume cha sheria wajitokeze katika ofisi za mamlaka hiyo ili kupata vibali halali au kwa wanaohitaji kumiliki wanaruhusiwa
Katika mahojiano hayo, afisa huyo pia alizungumzia suala la uwindaji wa kitalii akieleza kuwa ni moja ya vyanzo vya mapato kwa serikali na jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi. Alisisitiza kuwa uwindaji huo hufanywa kwa kufuata taratibu za kisheria.

Kwa upande wake Adelard Tesha Afisa Utalii Kijereshi ameeleza utalii unaofanyika ndani ya pori la akiba Kijereshi akitoa wito kwa watu kupenda kutembelea vivutio vya utalii kwani kuna faida kwao na kwa uchumi wa nchi.
Hata hivyo Judith Bulugu Afisa mahusiano Bunda kutoka TAWA kanda ya ziwa amewatoa hofu wananchi kuhusu bei za viingilio vya kutembelea vivutio vya utalii.