Mazingira FM
Mazingira FM
29 September 2025, 1:27 pm

Sikiliza makala haya maalumu kuhusu uelewa wa jamii kuhusu uzazi wa mpango hatua ya kujenga jamii na uchumi.
Na Dinnah Shambe
Katika jamii nyingi, suala la uzazi wa mpango limeendelea kuwa jambo lenye mjadala mkubwa, hasa kutokana na mitazamo tofauti ya kitamaduni, kijamii, na kidini. Watu wengi bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu maana, umuhimu na faida za uzazi wa mpango. Hali hii huathiri kwa kiasi kikubwa ustawi wa familia na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Katika makala haya ya dakika 15 tumezungumza na jamii kujua mtizamo wao kuhusu Uzazi wa mpango ambao ni haki ya msingi ya kila mtu inayomuwezesha mwanamke au mwanaume kupanga idadi ya watoto wanaotaka, muda wa kupata mtoto mwingine, na aina ya maisha wanayoyapanga kama familia