Mazingira FM
Mazingira FM
26 September 2025, 1:02 pm

Katika uchaguzi huu hakuna kupita bila kupingwa kwa kuwa sheria inaelekeza kura ya ndiyo na hapana kwa mgombea ambaye iwe ni jimbo au kata hana mpinzani.
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa wananchi kutumia haki yao ya kikatiba kuhakikisha wanapiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa October 29 mwaka huu ili kuchagua viongozi wanaowataka,
Hayo yamesemwa na Anthony Mayunga ambaye ni Afisa habari wa shirika la Getiasamo Paralegal Organization alipokuwa akizungumza na Radio Mazingira FM kupitia kipindi cha Asubuhi leo .
Mayunga amesema yapo mambo kadhaa ambayo mpiga kura anatakiwa kuyazingatia au mtu yeyote anayetaka kupiga kura anatakiwa kuwa na sifa ikiwa ni pamoja na lazima awe amejiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura, awe raia wa Tanzania miongoni mwa sifa zingine.
Pia amesema katika uchaguzi huu hakuna kupita bila kupingwa kwa kuwa sheria inaelekeza kura ya ndiyo na hapana kwa mgombea ambaye iwe ni jimbo au kata hana mpinzani.
Kwa upande wake Hamis Marwa msaidizi wa kisheria amesema kuelekea uchaguzi tume huru ya taifa ya uchaguzi imeandaa utaratibu mzuri ambao wananchi na wapiga kura wanatakiwa kuufuata hasa siku yenyewe ya kupiga kura ikiwemo kuwa na nguo au kito chochote kinachoashiria kuwa wewe ni mfuasi wa chama chochote cha siasa.