Mazingira FM

Dawati la uwezeshaji biashara TRA lawaletea nafuu wafanyabiashara

26 September 2025, 6:16 pm

Ruth Kisinga, Afisa msaidizi wa kodi mkoa wa Mara

Ruth Kisinga afisa msaidizi wa kodi mkoa wa Mara Ruth amesema kuwa hapo nyuma hapakuwa na mahusiano mazuri kati ya TRA na walipa kodi hivyo dawati hili limekuwa msaada na kuleta mahusiano mazuri baina  yao.

Na Teddy Thomas

Imeelezwa kwamba dawa la  uwezeshaji biashara ndani ya TRA limekuwa msaada na daraja kati ya mamlaka  ya mapato  Tanzania TRA na wafanyabiashara pamoja na wajasiriamali wadogo katika kutatua changamoto na hatari zinazopatikana kwenye biashara.

Hayo yamesemwa leo September 25, 2025 na Ruth Kisinga afisa msaidizi wa kodi mkoa wa Mara kwenye kipindi maalumu kilichorushwa na Mazingira fm.

 Aidha Ruth amesema kuwa hapo nyuma hapakuwa na mahusiano mazuri kati ya TRA na walipa kodi hivyo dawati hili limekuwa msaada na kuleta mahusiano mazuri baina  yao.

Sauti ya Ruth Kisinga afisa msaidizi wa kodi mkoa wa Mara

Sambamba na hayo Ruth ameeleza lengo la kuanzishwa dawati  hilo ni kuhakikisha linatoa  ushauri kuhusu ulipaji kodi, kuunganisha wafanyabiashara na wadau wakutoa mikopo, na namna ya urasimishaji wa biashara.

Sauti ya Ruth Kisinga afisa msaidizi wa kodi mkoa wa Mara

Hata hivyo Ruth amesma TRA haipo kwaajili ya kuua biashara ya mtu isipokuwa ipo kwaajii ya kumuwezesha mfanyabiashara au mjasiriamali biashara yake inakuwa

Sauti ya Ruth Kisinga afisa msaidizi wa kodi mkoa wa Mara

Dawati la uwezeshaji biashara ndani ya TRA limezinduliwa kitaifa mwezi wa 8 mwaka 2025 na limendelea kufanya kazi kila mikoa  na kwa mkoa wa Mara mpaka sasa utekelezaji wake unaonesha ufanishi  katika kuhudumia wateja.