Mazingira FM
Mazingira FM
25 September 2025, 11:31 pm

Katibu wa NEC Uchumi na Fedha wa CCM Taifa, Ndg. Joshua Chacha Mirumbe awaomba wananchi kumuunga mkono Dkt. Samia kwa kura, pamoja na mgombea mwenza Dkt. Emmanuel Nchimbi, mgombea ubunge Ndg. Boniphace Getere na wagombea udiwani wa CCM.
Na Thomas Masalu
Katibu wa NEC Uchumi na Fedha wa CCM Taifa, Ndg. Joshua Chacha Mirumbe, amewataka wananchi wa Wilaya ya Bunda, kujivunia kuaminiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupata viongozi wa kitaifa kutoka eneo hilo, akisema ni fursa ya kuwasilisha changamoto kwa urahisi.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni kijijini Kihumbu, Kata ya Hunyari, Mirumbe aliwaomba wananchi kumuunga mkono Dkt. Samia kwa kura, pamoja na mgombea mwenza Dkt. Emmanuel Nchimbi, mgombea ubunge Ndg. Boniphace Getere na wagombea udiwani wa CCM.
