Mazingira FM

Mirumbe: CCM imeandaa ilani kila mkoa na hitaji lake

25 September 2025, 9:40 am

Katibu wa NEC wa Uchumi na Fedha wa CCM Taifa, Ndg. Joshua Chacha Mirumbe

Ilani ya mkoa ya mkoa wa Mara imegusia mambo yote muhimu ikiwemo, afya, maji na miundombinu mingine.

Na Thomas Masalu

Katibu wa NEC wa Uchumi na Fedha wa CCM Taifa, Ndg. Joshua Chacha Mirumbe, amewakumbusha wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Tarime kuwa wanalo jukumu kubwa katika kipindi hiki cha uchaguzi kuhakikisha wanatimiza wajibu wao,

Amesema jukumu hilo kama ilivyoelekezwa katika Ibara ya 5 ya Katiba ya Chama, inayowataka kusimamia uchaguzi kwa ufanisi na kuhakikisha ushindi wa chama.

Ndg. Mirumbe ametoa kauli hiyo tarehe 24 Septemba 2025 katika ukumbi wa CMG mjini Tarime, wakati akizungumza na Wanachama na Viongozi wa CCM wa Wilaya ya Tarime, Mkoa wa Mara.

Aidha, ameeleza kuwa hakuna Mgombea aliyechaguliwa na mtu binafsi, bali Wagombea wote wa nafasi za Udiwani na Ubunge wameteuliwa na Chama chenyewe kwa kuzingatia taratibu na vigezo vilivyowekwa.

Sauti ya Katibu wa NEC wa Uchumi na Fedha wa CCM Taifa, Ndg. Joshua Chacha Mirumbe

Katika hotuba yake, Ndg. Mirumbe ametumia fursa hiyo kuwaeleza wanachama kuhusu mambo yaliyomo katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM, hususan yale yanayohusu Wilaya ya Tarime na Mkoa wa Mara kwa ujumla.

Amefafanua zaidi kuhusu masuala yaliyogusiwa kwenye Ilani, ikiwemo maendeleo katika sekta ya elimu, afya, miundombinu na huduma mbalimbali za kijamii.

Sauti ya Katibu wa NEC wa Uchumi na Fedha wa CCM Taifa, Ndg. Joshua Chacha Mirumbe