Mazingira FM

Waitara akabidhiwa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030

24 September 2025, 11:49 am

Katibu wa NEC Uchumi na Fedha wa CCM, Ndugu Joshua Chacha Mirumbe, akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030 Mgombea wa ubunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Ndugu Mwita Mwikwabe Waitara,picha na Thomas Masalu

Ndugu Joshua Chacha Mirumbe asema CCM imedhamiria kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli kupitia utekelezaji wa miradi ya kimkakati kwenye sekta za kilimo, elimu, afya, miundombinu na ajira kwa vijana.

Na Thomas Masalu

Katibu wa NEC Uchumi na Fedha wa CCM, Ndugu Joshua Chacha Mirumbe, amemkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030 Mgombea wa ubunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Ndugu Mwita Mwikwabe Waitara, katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Muriba leo September 23.

Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye mkutano

‎Katika hotuba yake, Ndugu Mirumbe ameeleza kuwa Ilani hiyo ni nyenzo muhimu inayobeba dira ya maendeleo ya wananchi wa Tarime na Taifa kwa ujumla.

‎‎Amesisitiza kuwa CCM imedhamiria kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli kupitia utekelezaji wa miradi ya kimkakati kwenye sekta za kilimo, elimu, afya, miundombinu na ajira kwa vijana.

Sauti ya Katibu wa NEC Uchumi na Fedha wa CCM, Ndugu Joshua Chacha Mirumbe