Mazingira FM

Joshua Mirumbe:Tupeni kura zote kuendeleza maendeleo kata ya muriba

24 September 2025, 11:37 am

Ndg.Joshua Chacha Mirumbe, Katibu wa NEC Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi CCM,akimnadi mgombea ubunge jimbo la Tarime Vijijini,picha na Thomas Masalu

Ndg.Mirumbe Katibu wa NEC Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa amesema October 29 mwaka huu, wananchi wakampigie kura Daktari Samia Suluhu Hassan pamoja na Mgombea Ubunge Mwita Waitara na Wagombea udiwani wote wa CCM.

Na Thomas Masalu

Wananchi wa Kata ya Muriba, Jimbo la Tarime Vijijini, Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara, wametakiwa kuwachagua Wagombea wote wa CCM kwa kura zote ili kuendeleza kasi ya maendeleo.

Wito huo umetolewa na Ndg.Joshua Chacha Mirumbe, Katibu wa NEC Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi CCM, wakati wa mkutano wa kampeni wa kumnadi Mgombea ubunge Mwita Mwikwabe Waitara pamoja na madiwani.

Sauti ya Ndg.Joshua Chacha Mirumbe, Katibu wa NEC CCM

Ndg.Mirumbe amesema October 29 mwaka huu, wananchi wakampigie kura Daktari Samia Suluhu Hassan pamoja na Mgombea Ubunge Mwita Waitara na Wagombea udiwani wote wa CCM.

Katika hatua nyingine, wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Muriba, Jimbo la Tarime Vijijini, wametakiwa kuvunja makundi na kuwa wamoja katika kuwaunga mkono wagombea wa CCM.

Katibu wa NEC Uchumi na Fedha wa CCM, Joshua Chacha Mirumbe, amesema huu si wakati wa makundi bali mshikamano kwa ajili ya ushindi wa CCM

Amesema Wagombea wa CCM ni madhubuti na wana nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi.

Sauti ya Ndg.Joshua Chacha Mirumbe, Katibu wa NEC CCM

Kwa upande wake, Mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara, ameeleza mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka mitano iliyopita wakati wa uongozi wake wa awali, huku akieleza matumaini na mwelekeo wa kimaendeleo endapo atapewa ridhaa ya wananchi kwa mara nyingine.

Sauti ya mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara