Mazingira FM
Mazingira FM
24 September 2025, 11:02 am

Katibu wa NEC wa Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa,Ndg.Joshua Mirumbe awaeleza wananchi kuhusu dhamira ya chama katika kuwaletea maendeleo endelevu na kueleza kwa kina sababu za CCM kumteua Ndg. Waitara kugombea Ubunge katika jimbo hilo.
Na Thomas Masalu
Katibu wa NEC wa Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Ndg. Joshua Chacha Mirumbe, ameendelea na ziara yake katika Mkoa wa Mara kwa kushiriki kikamilifu katika kampeni za kumnadi Mgombea Ubunge wa CCM katika Jimbo la Tarime Vijijini, Ndg. Mwita Waitara.
Mkutano umefanyika 23 September 2025 katika Kata ya Mwema – Kubiterere Jimbo la Tarime Vijijini Mkoa wa Mara, Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa CCM Mkoa, Wilaya ,Kata, Matawi, Wanachama pamoja na Wagombea wa nafasi ya Ubunge, Udiwani na Madiwani wa Viti Maalum.
Ndg. Mirumbe aliwaeleza wananchi kuhusu dhamira ya chama katika kuwaletea maendeleo endelevu na kueleza kwa kina sababu za CCM kumteua Ndg. Waitara kugombea Ubunge katika jimbo hilo.
“Tuna imani kubwa na Ndg. Mwita Waitara kutokana na uwezo wake, uzoefu, na utayari wa kuwahudumia wananchi.
Amekuwa kiongozi wa mfano katika nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika serikalini na ndani ya chama.
Tunahitaji sauti madhubuti kama yake bungeni ili kushirikiana na Serikali kuwaletea maendeleo watu wa Tarime Vijijini,” alisema Ndg. Mirumbe
