Mazingira FM

Tamka: Kata ya Balili ni eneo la utalii na uwekezaji

23 September 2025, 8:04 pm

Mgombea udiwani kupitia chama cha Mapinduzi CCM kata ya Balili  Thomas Tamka Chikongoe akiwa na viongozi wa chama kata ya balili kwenye uzinduzi wa kampeni,picha na (Catherine Msafiri)

Mgombea udiwani kupitia chama cha Mapinduzi CCM kata ya Balili  Thomas Tamka Chikongoe amuomba mgombea ubunge wa CCM jimbo la Bunda kuhakikisha atakapo apishwa kuwa mbunge asaidie kujenga ofisi za TANAPA,kuongeza taa za barabarani na kukamilisha  ujenzi wa zahanati

Na Catherine Msafiri

Mgombea udiwani kupitia chama cha Mapinduzi CCM kata ya Balili  Thomas Tamka Chikongoe amezindua rasmi kampeni za uchaguzi katika kata hiyo huku akiweka bayana yaliofanywa na serikali kama ujenzi wa madarasa yalioghalimu shilling bilion 200.

Chikongoe amezungumza hayo kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi katika kata hiyo ambapo amefafanua kuwa chama cha mapinduzi kinatekeleza ilani ya chama hivyo wananchi wachague viongozi wa chama hicho

Sauti ya mgombea udiwani kupitia chama cha Mapinduzi CCM kata ya Balili  Thomas Tamka Chikongoe

Aidha amebainisha kuwa kata ya balili ni eneo la kiuwekezaji hivyo amemuomba mgombea ubunge wa CCM jimbo la Bunda kuhakikisha atakapo apishwa kuwa mbunge asaidie kujenga ofisi za TANAPA,kuongeza taa za barabarani na kukamilisha  ujenzi wa zahanati.

Sauti ya mgombea udiwani kupitia chama cha Mapinduzi CCM kata ya Balili  Thomas Tamka Chikongoe
Baadhi ya wakazi wa kata ya Balili wakiwa kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi

Akizungumza mbele ya wakazi wa kata ya Balili iliopo halmashauri ya mji wa Bunda mgombea ubunge wa jimbo la Bunda mjini Ester Amos Bulaya ameahidi kushughulikia changamoto za wakazi wa kata hiyo ikiwemo barabara na usimamizi mzuri wa miradi ya maji .

Sauti ya mgombea ubunge wa jimbo la Bunda mjini Ester Amos Bulaya

Hata hivyo ameongeza kuwa suala la taa amelibeba na atalishughulikia ili kuwaweka wakazi wa balili salama na kuepukana na ajali za barabarani na tembo.

Sauti ya mgombea ubunge wa jimbo la Bunda mjini Ester Amos Bulaya