Mazingira FM

Bulaya: Sitowaacha watoto wa mazingira magumu

22 September 2025, 7:54 pm

Mgombea ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini Ester Amos Bulaya akiwa na Mgombea udiwani kata ya Bunda stoo, Flavian Chacha Nyamigeko,picha na Adelinus Banenwa

Ester Bulaya ameeleza dhamira yake ya kuendeleza utaratibu ulioanzishwa na mtangulizi wake, RobartChacha Maboto, wa kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupata elimu

Na Catherine Msafiri,

Mgombea ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ester Amos Bulaya, ameahidi kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya miundombinu na elimu endapo atapewa ridhaa ya kuwatumikia wananchi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Akihutubia maelfu ya wakazi wa Kata ya Bunda Stoo katika uzinduzi wa kampeni za udiwani, Ester amesema kwa kipindi kijacho, kipaumbele chake cha kwanza kitakuwa ni usimamizi madhubuti wa ujenzi wa barabara kwa viwango vya juu, akiahidi kuwa hakuna mkandarasi atakayepewa nafasi ya kufanya kazi chini ya kiwango.

Sauti ya mgombea ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini (CCM), Ester Amos Bulaya

Mbali na miundombinu, Ester Bulaya ameeleza dhamira yake ya kuendeleza utaratibu ulioanzishwa na mtangulizi wake, RobartChacha Maboto, wa kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupata elimu na mahitaji ya msingi ya shule.

Sauti ya mgombea ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini (CCM), Ester Amos Bulaya

Bulaya ameongeza kuwa maendeleo ya kweli hayawezi kupatikana bila miundombinu bora na uwekezaji katika elimu, huku akiwataka wananchi wa Bunda Mjini kufanya maamuzi sahihi kwa kumchagua kiongozi mwenye dira, uthubutu na moyo wa kuwahudumia.

Baadhi ya wakazi wa kata ya Bunda stoo wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni,picha na Adelinus Banenwa