Mazingira FM

Nyamigeko azindua kampeni, aeleza mafanikio ya miaka mitano Bunda stoo

22 September 2025, 7:43 pm

Mgombea udiwani wa chama cha mapinduzi (CCM) katika kata ya Bunda stoo, Flavian Chacha Nyamageko akiwa kwenye uzinduzi,picha na Adelinus Banenwa

Mgombea udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Bunda Stoo, Flavian Chacha Nyamigeko, amezindua rasmi kampeni zake za uchaguzi kwa kueleza mafanikio ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo 2020-2025

Na Catherine Msafiri,

Mgombea udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kata ya Bunda stoo, Flavian Chacha Nyamigeko, amezindua rasmi kampeni zake za uchaguzi kwa kueleza mafanikio ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo, Nyamigeko amesema uongozi wake umetatua changamoto nyingi za kijamii kwa kushirikiana na wananchi, ikiwa ni pamoja na kuimarisha huduma za elimu, maji na afya.

Ametaja mafanikio hayo kuwa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya tatu za sekondari ambazo zimepunguza msongamano wa wanafunzi na kuongeza upatikanaji wa elimu kwa watoto wa kata hiyo.

Aidha, amesema miradi kadhaa ya maji safi na salama imekamilika, na usambazaji wa huduma hiyo kwa mitaa iliyokuwa havijafikiwa awali.

Sauti ya mgombea udiwani kata ya Bunda stoo, Flavian Chacha Nyamigeko
Baadhi ya wakazi wa kata ya Bunda stoo wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni,picha na Adelinus Banenwa

Katika sekta ya afya, Nyamigeko amesema kata hiyo imenufaika na ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bunda, ambayo sasa inatoa huduma kwa wakazi wa maeneo mbalimbali ya mji huo.

Ameeleza kuwa dhamira yake ya kuomba ridhaa ya kuendelea ni kuhakikisha miradi iliyopo inakamilika kwa wakati na kuanzisha mingine kwa kushirikiana na wananchi.

Sauti ya mgombea udiwani kata ya Bunda stoo, Flavian Chacha Nyamageko