Mazingira FM
Mazingira FM
18 September 2025, 5:49 pm

Wakazi wa mtaa huo wa Miembeni wameishukuru Serikali na mamlaka ya maji Bunda kwa kuwakumbuka kuwafikishia huduma ya maji safi
Na Adelinus Banenwa
Zaidi ya kaya 125 kata ya Bunda stoo mtaa wa miembeni maarufu Ukanda wa Gaza kunufaika na mradi wa usambazji maji kutoka mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Bunda BUWSSA.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka hiyo Bi Esther Gilyoma wakati akikabidhi mabomba kwa wakazi hao ambayo yametolewa na serikali kupitia mamlaka hiyo huku akiongeza kuwa kwa sasa mamlaka inaendelea na miradi mitano ukiwemo mradi wa Maji taka,Mradi wa usambazaji maji wa Kisangwa, Mradi wa usambazaji maji Wariku, mradi wa maji Nyamuswa na mradi wa kupambana na upotevu wa maji wa bomba kuu kwenda mlima kaswaka.

Aidha Bi Gilyoma amesema mradi huo wa usambazaji maji eneo la Ukanda wa Gaza mtaa wa Miembeni utakuwa na urefu wa zaidi ya kilometa 2 na kutakuwa na vituo viwili vya kuchotea maji yaani DPs.
Kwa upande wao wakazi wa mtaa huo wa Miembeni wameishukuru Serikali na mamlaka ya maji Bunda kwa kuwakumbuka kuwafikishia huduma ya maji safi kwa kuwa tangu uhuru eneo hilo halijawahi kupata huduma ya maji safi

Wakazi hao wamesema wako tayari kushirikiana na BUWSSA hata kuchimba mitaro ili huduma hiyo iweze kuwafikia kwa haraka.