Mazingira FM
Mazingira FM
15 September 2025, 6:32 pm

Afisa Kilimo kutoka Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Mara Pamba Mara Cooperative Fikiri Maregesi Mauna ameiomba serikali kufufua viwanda vilivyopo mkoani Mara.
Na Catherine Msafiri,
Afisa Kilimo kutoka Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Mara Pamba Mara Cooperative Fikiri Maregesi Mauna kinachoshughulikia zao la pamba pamoja na mazao mchanganyiko ya kimkakati amewasii wakulima wa mkoa wa Mara kuchangamkia fursa ya mazao ya kimkakati yaliyoanzishwa mkoani Mara kwa manufaa ya wakulima kama dengu ,mbaazi,choroko ,ufuta ,mahindi pamoja na tumbaku.
Ameyasema hayo leo 15 Sept 2025 wakati akizungumza na mazingira fm kwenye banda la shirika hilo lililopo kwenye viwanja vya mwenge wilayani Butiama yanapofanyika maadhimisho ya Mara day ambapo amesema kwasasa serikali imeboresha soko la mazao hayo kwa kupitia mfumo wa sitakabadhi ghalani
Aidha ameiomba serikali kufufua viwanda vilivyopo mkoani Mara ili kuwawezesha katika kuchakata mazao hayo ya kimkakati huku akibainisha masoko yaliyopo kwaajili ya mazao hayo na kuwasii wakulima kuacha kuuza mazao yao kwa vipimo visivyo sahihi bali wapime kwa kilo(mzani)