Mazingira FM
Mazingira FM
14 September 2025, 8:29 pm

Katibu wa NEC Uchumi na Fedha (MCC) Ndg. Joshua Mirumbe leo tarehe 14 Sept 2025 amezindua kampeni za uchaguzi kwa wilaya ya Maswa yenye majimbo mawili ya uchaguzi ambayo ni Maswa. Mashariki na Maswa Magharibi.
Akizungumza na wananchi wa Jimbo la Maswa Mashariki katka Viwanja vya Ipililo kwa Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Dkt George Venance Lugomela Ndugu Mirumbe amewataka waliotia nia wote kuhakikisha wanavunja Makundi na wanashiriki kikamilifu kutafuta kura za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi, wabunge katika majimbo yote mawili na madiwani wa CCM katika Kata zote 36 za Wilaya ya Maswa.

Ndugu Mirumbe amesema kuna sababu za kutosha kumchagua Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa aliyoifanya akimtaja kuwa Kiongozi shupavu, Jasiri na Mleta maendeleo akiwakumbusha wakazi wa Maswa kwamba wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi Dkt Samia alihaidi ndani ya siku 100 baada ya kuchaguliwa atashughulikia bima za afya pia ataongeza ajira za watumishi katika sekta ya Afya na Elimu.
Ndugu Mirumbe ameongeza kuwa kwa Wilaya ya Maswa katika Sekta ya Afya ametoa fedha za kujenga kituo cha Afya na Zahanati, upande wa Barabara za TARURA na zingine za Lami, pia Upanuzi wa mtandao wa Maji katika Mradi wa maji wa ziwa Victoria kwenda Bariadi na baadae Bariadi kwenda Maswa pia amewakumbusha kuwa Wilaya ya Maswa ni wanufaika wa mradi wa SGR kwa kuwa na kituo cha Reli eneo la Marampaka hivyo endapo wataichagua CCM itakamilisha mradi huo wa SGR Ambao kwa sasa kipande kinachojengwa ni kutoka Dodoma kwenda Isaka na Mwanza.

Katika mkutano huo waliokuwa watiania wote wa Ubunge katika Majimbo hayo wamekubali kuvunja makundi na kuungana kwa pamoja na wateule kutafuta kura za ushindi wa Rais, Wabunge na Madiwa wa CCM katika Uchaguzi mkuu wa October 2025.