Mazingira FM

Uhamiaji Bunda yakaribisha wananchi kupata elimu

14 September 2025, 10:33 am

Mrakibu wa Uhamiaji, Sadikiel Jonas Mhomboje, Afisa Uhamiaji wa Wilaya ya Bunda,

Mhomboje amesisitiza kuwa zoezi la uchaguzi linawahusu Watanzania pekee, na kwamba raia wa kigeni hawaruhusiwi kushiriki kwa namna yoyote ile.

Na Edward Lucas

Wananchi wametakiwa kutokuwa na hofu kutembelea ofisi za Uhamiaji kwa ajili ya kuuliza na kupata taarifa mbalimbali zinazohusu masuala ya uhamiaji, ili kuendelea kudumisha amani na mshikamano wa kitaifa.

Wito huo umetolewa leo na Mrakibu wa Uhamiaji, Sadikiel Jonas Mhomboje, Afisa Uhamiaji wa Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, wakati akizungumza na Radio Mazingira FM katika kipindi cha Ufahamu wa Sheria kuhusu mada ya Ulowezi na Uhamiaji Haramu.

Mrakibu wa Uhamiaji, Sadikiel Jonas Mhomboje, Afisa Uhamiaji wa Wilaya ya Bunda,

Mhomboje amesema wananchi hawapaswi kuwa na dukuduku, bali watumie ofisi za uhamiaji kupata ufafanuzi wa mambo mbalimbali, kwani kufanya hivyo kutasaidia kupunguza sintofahamu na kudumisha utulivu katika jamii.

Sauti ya Mrakibu wa Uhamiaji, Sadikiel Jonas Mhomboje, Afisa Uhamiaji wa Wilaya ya Bunda,

Aidha, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Mhomboje amesisitiza kuwa zoezi la uchaguzi linawahusu Watanzania pekee, na kwamba raia wa kigeni hawaruhusiwi kushiriki kwa namna yoyote ile.

Sauti ya Mrakibu wa Uhamiaji, Sadikiel Jonas Mhomboje, Afisa Uhamiaji wa Wilaya ya Bunda,