Mazingira FM
Mazingira FM
13 September 2025, 6:41 am

Wanauwezo wa kujenga hoja, kusimamia masilahi ya Taifa, ujenzi wa Uchumi Imara na huduma za jamii kamavile miundombinu, Elimu na Afya.
Na Adelinus Banenwa
Ndugu Joshua Chacha Mirumbe. Katibu wa NEC Uchumi na Fedha na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa amewataka wanachama wa chama hicho kuondoa dhana ya mgombea kupita bila kupingwa akisema lazima wajitokeze siku ya uchaguzi kwenda kupiga kura
Amesema suala la kupita bila kupingwa kwa sasa halipo hata kama mgombea amebaki peke yake kwa mujibu wa sheria iliyotungwa bungeni unaweza kukuta kura za hapana ni nyingi ukilinganisha na kura za ndiyo hivyo ni wajibu wa wanachama kuhakikisha wanakwenda kupiga kura kwa Rais Mbunge na Diwani walioletwa na chama cha mapinduzi.
Mirumbe ameongeza kuwa CCM kama chama cha siasa kwa wakati huu wanayo kazi moja tu ya kushinda uchaguzi na kurudi madarakani.
Ndugu Mirumbe ameyasema hayo leo tarehe 12 Sept 2025 akiwa kata ya Sazira Bunda mjini alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Chama,Jumuiya na Wanachama wa CCM wa Kata ya Saziara Katika Jimbo La Bunda Mjini

Aidha Ndugu mirumbe amesema mchakato uliofanyika katika kuwapata wagombea ulifanyika kwa weledi na waleoteuliwa katika nafasi za udiwani na ubunge vikao vilijiridhisha hivyo haitakiwi mtu yeyote kuwa na mashaka juu ya uteuzi wa wagombea hao kwa ngazi iwe ya udiwani ama ubunge.
Pia Ndugu Joshua Chacha Mirumbe amewanadi wagombea wa CCM wa kwanza ni Dkt Samia Suluhu Hassani na Balozi Dkt Emanuel John Nchimbi katika nafasi ya Rais, Nafasi ya Mbunge Ester Amos Bulaya na Udiwani Michael Kweka amesema wanauwezo wa kujenga hoja, kusimamia masilahi ya Taifa, ujenzi wa Uchumi Imara na huduma za jamii kamavile miundombinu, Elimu na Afya.