Mazingira FM
Mazingira FM
11 September 2025, 8:57 pm

Utajiri uliopo nchini Tanzania kwa wingi la rasilimali zilizopo yakiwemo madini, mito maziwa na bahari, ardhi yenye rutuba miongoni mwa rasilimali zingine
Na Adelinus Banenwa
Mgombea urais kupitia chama cha ukombozi wa umma CHAUMA Salumu Mwalimu amesema endapo atachaguliwa katika uchaguzi wa mwezi October kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania atahakikisha anajenga viwanda mkoani Mara na kuimarisha sekta ya kilimo ili kukuza ustawi wa wananchi na kuongeza ajira.

Mwalimu ameyasema hayo leo katika mkutano wake wa kampeni wilayani Bunda uliofanyika stendi ya zamani Mjini Bunda ikiwa ni mwendelezo wa kunadi sera za chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu.
Mbali na ahadi hizo Mwalimu amebainisha suala la utajiri uliopo nchini Tanzania kwa wingi la rasilimali zilizopo yakiwemo madini, mito maziwa na bahari, ardhi yenye rutuba miongoni mwa rasilimali zingine ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuwakwamua wananchi kiuchumi na kuondoa umasikini miongoni mwa watanzania.
