Mazingira FM

Plastiki, nguo chakavu, mabaki ya chakula fursa mpya ya ajira

8 September 2025, 10:54 am

Picha inayoonesha taka zikiwemo za plastiki zinavyochafua mazingira

Vijana changamkieni fursa za ajira kupitia urejelezaji wa taka kama plastiki, chuma, vitambaa au nguo zilizoisha na mabaki ya chakula ili kusaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira.

Na Catherine Msafiri,

Tanzania imekuwa na changamoto ya uchafuzi wa mazingira kwa hivi karibuni hususani maeneo ya mijini kutokana na ongezeko la watu, hali inayopelekea kuongezeka kwa uzalishaji wa taka kutoka tani 14.4 hadi 20.7 milioni kwa mwaka kwa mujibu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Wito umetolewa kwa vijana kuchangamkia fursa za ajira kupitia urejelezaji wa taka kama plastiki, chuma, vitambaa au nguo zilizoisha na mabaki ya chakula ili kusaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira.
Wito huo umetolewa na mhamasishaji wa elimu ya mazingira Flavian Ernest Nyanza wakati akizungumza kwenye kipindi cha Uhifadhi na Utalii cha Mazingira FM 7 Sept 2025 kilichozungumzia namna taka zinavyoweza kurejelezwa ili kuhifadhi mazingira.

Sauti ya Flavian Nyanza mhamasishaji wa elimu ya mazingira

Kwa upande wake Bi. Sara Yohana Mgaya kutoka taasisi ya GEPM ameeleza kuwa matumizi ya taka za plastiki kama mifuko inaweza kuhatarisha afya ya mimea kwa kuweka matabaka ardhini. Ameshauri utunzaji wa taka kwa kuzitenganisha ili kusaidia katika kurejeleza na kupunguza uchafuzi wa mazingira.

Sauti ya Sara Mgaya kuhusu taka za plasitiki

Hata hivyo hivi karibuni NEMC limezindua kampeni ‘NEMC USAFI CAMPAIGN’ yenye lengo la kuchochea mabadiliko chanya ya kijamii, kiuchumi na kiafya kwa kuzingatia usimamizi na uhifadhi wa mazingira.