Mazingira FM
Mazingira FM
5 September 2025, 6:02 am

Nitahakikisha nafufua viwananda vya Musoma na kujenga bandari ili kusaidia kupatikana meli kubwa itakayofanya safari zake kati ya Musoma, Kenya na Uganda.
Na Adelinus Banenwa
Mgombea Ubunge jimbo la Musoma Mjini kupitia tiketi ya chama cha ACT Wazalendo Ndg. John Rugulu Kasereka amesema endapo wananchi watampa ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo katika uchaguzi wa mwaka huu, atahakikisha anafufua viwananda vya muteksi na kusaidia kupatikana meli kubwa itakayofanya safari zake kati ya Musoma, Kenya na Uganda.
Kasereka ameyasema hayo leo Sept 4, 2025 katika mahojiano maalumu na Radio Mazingira Fm iliyotaka kujua kwa nini ameamua kugombea ubunge wa jimbo hilo na kipi kipaumbeke chake.
Mbali na vipaumbele hivyo pia amehaidi kuufungua mji wa Musoma kiuchumi ili kila mtu kwa shughuli yake apate maendeleo huku akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kampeni zake anazotarajia kuzizindua Sept 10, 2025.
Kasereka ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanapiga kura siku ya tarehe 29 oct 2025