Mazingira FM
Mazingira FM
5 September 2025, 5:57 am

Lengo la chama hicho ni kuwajaza wananchi pesa kwa kuimarisha sekta mbalimbali ili kukuza uchumi na kuwawezesha watu kujiingizia kipato.
Na Adelinus Banenwa
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha United Democratic Party (UDP), Saum Hussein Rashid, amesema lengo la chama hicho ni kuwajaza wananchi pesa kwa kuimarisha sekta mbalimbali ili kukuza uchumi na kuwawezesha watu kujiingizia kipato na hivyo kuwa na maisha bora.
Amesema hayo Septemba 3, 2025, wakati wa kampeni za chama hicho uliofanyika katika stendi ya zamani mjini Bunda Saum mesema endapo atapata ridhaa ya kuwa Rais atahakikisha anakuza sekta ya kilimo kwani Watanzania wengi wanategemea kilimo katika kuendesha maisha yao.
Aidha, amesema vipaumbele vingine ni pamoja na kukuza viwanda kwa kujenga viwanda katika kila mkoa, hatua itakayosaidia kuongeza uzalishaji, ajira na ukuaji wa uchumi.

Kuhusu sekta ya afya, Saum amesisitiza kuwa kuimarisha huduma kutasaidia kujenga wananchi wenye afya bora, kwa kuwa afya bora ndiyo msingi wa maendeleo hivyo kuchangia maendeleo ya taifa, huku akiahidi elimu Bure mpaka chuo kikuu.
Suala la kuwajaza watu mapesa ikiwa bado ajenda kuu ya chama hicho hasa kwa kuwajengea mazingira mazuri ya wananchi kukua kiuchumi