Mazingira FM

Marufuku wanafunzi kucheza muziki|ngoma kwa kukata viuno Mara

2 September 2025, 7:20 pm

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Gerald Kusaya,

Uongozi wa mkoa unazielekeza halmashauri kuhakikisha wakurugenzi wanatekeleza na kufuatilia kwa ukaribu maagizo hayo katika shule zote ili yasipuuzwe.

Na Therezia Thomas

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Gerald Kusaya, amepiga marufuku wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo mkoani Mara kucheza ngoma na muziki kwa mtindo wa kukata viuno akisema aina hiyo ya uchezaji haiendani na maadili pamoja na mafunzo yanayotarajiwa kwa watoto wa umri huo.

Akizungumza leo, Septemba 2, 2025, katika kikao cha mapitio ya utekelezaji wa programu jumuishi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto MMMAM kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Kusaya amesema marufuku hiyo inaanza kutekelezwa mara moja.

Baadhi ya washiri wa kikao kutoka kwenye halmashauri za mkoa wa Mara

Amesema uongozi wa mkoa unazielekeza halmashauri kuhakikisha wakurugenzi wanatekeleza na kufuatilia kwa ukaribu maagizo hayo katika shule zote ili yasipuuzwe.

sauti ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Gerald Kusaya,

Katika hatua nyingine, Kusaya amezitaka halmashauri zote mkoani humo kuimarisha mpango wa lishe shuleni sambamba na kuendesha kampeni za uhamasishaji wa lishe bora majumbani.

Awali, taarifa zilizowasilishwa kutoka halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Mara zilionyesha kuwa tatizo la utapiamlo bado lipo, hususan kwa watoto wenye umri wa kuanzia miaka 0 hadi 8, hali inayosababisha wengine kupoteza maisha kutokana na ukosefu wa virutubishi muhimu mwilini.