Mazingira FM
Mazingira FM
2 September 2025, 7:11 pm

Chama cha DP wamejipanga kufungua kapeini na kuwaeleza watanzania juu ya sera zao na ilani yao hasa kwa upande wa afya ambapo matibabu yatakuwa ni bure na akinamama waliojifungua watalipwa.
Na Adelinus Banenwa
Makamu mwenyekiti wa chama cha Democratic Party yaani DP ndugu Christant Nyakitita amewataka watanzania wote wenye sifa ya kupiga kura kujitokeza siku ya tarehe 29 Oct 2025 kuchagua viongozi waowataka ili kutimiza wajibu wao wa kikatiba.
Nyakitita ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Redio Mazingira Fm kwa njia ya simu ambapo amesema wao kama chama cha DP wamejipanga kufungua kapeini na kuwaeleza watanzania juu ya sera zao na ilani yao hasa kwa upande wa afya ambapo matibabu yatakuwa ni bure na akinamama waliojifungua watalipwa.
Aidha Nyakitita amesema chama cha DP kinatarajia kufungua kampeini zao kitaifa mnamo tarehe 17 Sept 2025 mkoani Tabora kabla ya kuzunguka Tanzania nzima.
kwa upande wa mkoa wa Mara Nyakitita amesema awali chama hicho kilisimamisha wagombea watatu wa ubunge katika majimbo ya Musoma Mjini, Mwibara na Bunda Mjini, lakini kutokana an kanuni za sheria mpya ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani imebaki na wagombea wawili tu wa Musoma Mjini na wa Mwibara kutokana ana aliyekuwa amegombea jimbo la Bunda Mjini pia alikuwa amechukua fomu ya kuwania udiwani, na sheria ya uchaguzi inataka mtu agombee nafasi moja tu hivyo ilimlazimu mgombea huyo kuachana na ubunge na kubaki kama mgombea wa udiwani kwa kata ya Kabarimu