Mazingira FM

Dkt. Nchimbi aelezea yaliyotekelezwa Bunda chini ya Rais Samia

30 August 2025, 2:58 pm

Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM Balozi ,Dkt.Emmanuel Mchimbi akizungumza na wana Bunda,picha na Mwananchi

Dkt. Emmanuel Nchimbi amewaeleza wanabunda kuwa sera za mgombea urais Dkt.Samia zinalenga kuwaletea maendeleo wananchi na kuboresha kwa kiwango kikubwa.

Na Catherine Msafiri.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM na mgombea mwenza wa urais kupitia chama hicho Dkt.Emmanuel Mchimbi ameeleza mambo yaliotekelezwa katika wilaya ya Bunda chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ikiwamo ujenzi wa shule za sekondari mpya tatu huku akiweka wazi kuwa mpaka sasa Bunda ina jumla ya zahanati 34.

Dr.Nchimbi ameeleza hayo wakati akisalimiana na wakaazi wa Bunda 30 Augost 2025 eneo la stendi ya zamani Bunda alipowasili mkoani Mara Akiendelea na ziara yake mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa ajili ya Kufanya Kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Sauti ya Dr.Nchimbi akiongea na wananchi Bunda mkoani Mara

Aidha Dkt.Nchimbi amewaeleza wana Bunda kuwa sera za mgombea urais Dkt.Samia zinalenga kuwaletea maendeleo wananchi na kuboresha kwa kiwango kikubwa.

Miongoni mwao sera hizo alizozitaja ni pamoja na kutengeneza mfumo wa mawasiliano utakaosaidia wananchi kuweka kero zao kwenye mtandao na zitaonekana moja kwa moja kwa Rais Samia Suluhu Hassan na kupatiwa ufumbuzi pamoja na ajira mpya kwa walimu.

Sauti ya Dr.Nchimbi akieleza sera za mgombea urais chama cha mapinduzi

Kwa upande wake aliyekuwa mbunge wa jimbo la Bunda Robert Chacha Maboto amewaeleza wanabunda kuwa yeye ni mwanachama wa CCM na haitatokea akahama chama hicho , vilevile amesema kura watakazo piga wana Bunda ndizozitazowaletea maendeleo ndani ya Bunda.

Sauti ya Maboto aliyekuwa mbunge jimbo la Bunda

Naye mgombea ubunge jimbo la Bunda Ester Amos Bulaya akizungumza mbele ya Dkt.Nchimbi ameeleza namna ambavyo sera za CCM zitakavyojibu mahitaji ya wananchi wa Bunda hasa kwenye upande wa maji akitaja kuna mradi wa zaidi ya billion 10

Sauti ya Ester Bulaya mgombea ubunge jimbo la Bunda