Mazingira FM

Kifo cha Maria wa Karatu kilivyoleta utata kwa familia Tarime-Mara

27 August 2025, 8:36 pm

Picha ya marehemu Maria Vitalis Paul enzi za uhai wake

Mwandishi, Edward Lucas.

Familia mbili zimeingia kwenye mvutano kuhusu mahali pa kumzika Maria Vitalis Paulo (30), mwanamke anayedaiwa kuuawa na mume wake Mwita Ngere Mwita (37) kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Mrito, kata ya Kemambo, wilaya ya Tarime, mkoa wa Mara, ambapo marehemu aliishi na mumewe hadi mauti yalipomkuta.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mrito, Joseph Manga Gibao, amesema familia ya marehemu kutoka Karatu, mkoa wa Arusha, walifika kuchukua mwili wakikataa azikwe Tarime wakieleza kuwa aliuawa kikatili na mumewe.

Upande wa familia ya mume nao ulipinga uamuzi huo kwa maelezo kuwa kwa mila na desturi zao, mke aliyeolewa kwa mahari anapaswa kuzikwa kwao.

Baada ya mazungumzo marefu, familia zilikubaliana mazishi yafanyike Tarime, ingawa familia ya marehemu kutoka Arusha walisusia shughuli nyingine za mazishi.

Mwenyekiti kijiji cha Mrito Tarime, Joseph Gibao

Kwa mujibu wa Mwenyekiti Joseph Gibasi, Maria alifariki dunia tarehe 23 Agosti 2025 baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani kutokana na ugomvi wa wivu wa kimapenzi

Joseph Gibao, akisimulia zaidi tukio lililosababisha mauaji

Juhudi za kupata taarifa ya jeshi la polisi Tarime/Rorya bado hazijazaa matunda lakini kwa mujibu wa taarifa ya mwenyekiti Gibao ni kwamba mtuhumiwa alikamatwa na jeshi la polisi