Mazingira FM

Miradi ya 1.8b yafikiwa na mwenge Bunda DC

23 August 2025, 8:40 pm

Mhe Aswege Eneock Kaminyoge Mkuu wa Wilaya ya Bunda amepokea mwenge huo wa uhuru kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Serengeti Mhe Angelina Marco. Picha na Adelinus Banenwa

Mwenge wa uhuru kitaifa 2025 uliingia mkoa wa Mara kupitia wilaya ya Bunda kwa halmashauri ya mji wa Bunda tarehe 15 Aug 2025 na kuzunguka katika halmashauri zote tisa za mkoa wa Mara na leo Aug 23,2025.

Na Adelinus Banenwa

Mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2025 katika mkoa wa Mara zimetamatika leo katika halmashauri ya wilaya ya Bunda.
Mhe Aswege Eneock Kaminyoge Mkuu wa Wilaya ya Bunda amepokea mwenge huo wa uhuru kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Serengeti Mhe Angelina Marco.

Mhe Kaminyoge amesema jumla ya miradi yenye thamani ya shilling 1.8 Bilion kufikiwa na mwenge huo .

Sauti ya Aswege Eneock Kaminyoge Mkuu wa Wilaya ya Bunda
Wakimbiza mwenge kitaifa baada ya kukanyaga ardhi ya halamshauri ya Wilaya ya Bunda, Picha na Adelinus Banenwa

Kiongozi Wa mbio za mwenge kitaifa 2025 Ndugu Ismahil Ally Ussi ameipongeza halamashauri ya wilaya ya Bunda kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa viwango vinavyokubalika .
Akiwa shule ya msingi sababsita iliyoko kata ya Hunyari Halmashauri ya wilaya ya Bunda katika uzinduzi wa nyumba mbili za walimu zenye uwezo wa kukaa familia nne kwa maana ya 2in 1 Ndugu Ussi amesema

Sauti ya Kiongozi Wa mbio za mwenge kitaifa 2025 Ndugu Ismahil Ally Ussi
Kiongozi wa TAKUKURU Bunda akipokea mwenge ishara ya kufungua club ya kupinga rushwa shule ya msingi sabasita, Picha na Adelinus Banenwa

Ikumbukwe mwenge wa uhuru kitaifa 2025 uliingia mkoa wa Mara kupitia wilaya ya Bunda kwa halmashauri ya mji wa Bunda tarehe 15 Aug 2025 na kuzunguka katika halmashauri zote tisa za mkoa wa Mara na leo Aug 23,2025 wilaya ya Bunda imeupokea mwenge huo kupitia halmashauri ya wilaya ya Bunda kabla ya kesho Aug 24, 2025 kuukabidhi mwenge huo mkoani Mwanza kupitia wilaya ya Ukerewe.