Mazingira FM
Mazingira FM
21 August 2025, 6:15 pm

Mgombea wa udiwani kata ya Manyamanyama kupitia chama cha mapinduzi CCM ametangaza juu ya kuvunjwa kwa makundi yote yaliyokuwepo wakati wa kutafuta mgombea wa CCM kata.
Na Adelinus Banenwa
Mgombea wa udiwani kata ya Manyamanyama kupitia chama cha mapinduzi CCM ndugu Mathayo Juma Machilu ametangaza juu ya kuvunjwa kwa makundi yote yaliyokuwepo wakati wa kutafuta mgombea wa CCM kata ya Manyamanyama na badala yake kwa sasa walio kuwa watia nia wote kuungana kuhakikisha CCM inashinda kwenye uchaguzi mkuu wa tarehe 29 oct 2025

Mathayo ameyasema hayo leo tarehe 21 Aug 2025 baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo kwa msimamizi msaidizi watume huru ya taifa ya uchaguzi kwa kata ya Manyamanyama
Naye katibu wa chama hicho kwa kata ya Manyamanyama ndugu Clement Marco Rashid amewata wafuasi wa chama hicho na wananchi kujitokeza kwa wingi katiak kipindi cha kampeni kusikiliza sera zao huku akihaidi wao kufanya kampeni za kistaarabu biba kuvunja heshma ya mtu.