Mazingira FM

Wagombea wa CCM Sazira, Bunda mjini wavuta fomu INEC

20 August 2025, 5:30 pm

Mgombea wa udiwani kata ya Sazira kupitia chama cha mapinduzi CCM ndugu Michael Thomas Kweka akikabidhiwa fomu na msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Sazira

Wateule wa CCM kuwania udiwani waendelea kuchukua fomu kwenye ofisi za tume kwa wasimamizi wasaidizi kuomba kuteuliwa

Na Adelinus Banenwa

Mgombea wa udiwani kata ya Sazira kupitia chama cha mapinduzi CCM ndugu Michael Thomas Kweka amewashukuru wakazi anwanachama wa chama hicho waliomsindikiza kuchukua fomu ya kugombea udiwani wa kata ya sazira huku akihaidi kuendeleza yote aliyoyaanzisha ikiwemo miradi ya maendeleo endapo atachaguliwa kuwa diwani kwa kipindi cha pili

Kweka ameyasema hayo leo tarehe 20 Aug 2025 baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo kwa msimamizi msaidizi watume huru ya taifa ya uchaguzi kwa kata ya Sazira

Sauti ya Michael Thomas Kweka
Mgombea wa chama hicho cha mapinduzi kwa kata ya Bunda mjini ndugu Elias Mwita Samo akikabidhiwa fomu na msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Bunda Mjini

Wakati huo huo mgombea wa chama hicho cha mapinduzi kwa kata ya Bunda mjini ndugu Elias Mwita Samo amewataka wanachama wote wa CCM kuwa na umoja na mshikamano kuelekea uchaguzi mkuu huku akisisitiza kuwa endapo akishinda atahakikisha anaisimamia vizuri halmashauri na mikopo ya asilimia kumi inapatikana kwa walengwa

Samo pia ameyasema hayo leo baada ya kuchukua fomu ya kuwania udiwani wa kata hiyo kupitia CCM,

Sauti ya Elias Mwita Samo