Mazingira FM
Mazingira FM
19 August 2025, 8:39 pm

Makada wa CCM wapishana ofisi za wasimamizi wasaidizi wa tume kuchukua fomu za kuwania udiwani
Na Adelinu Banenwa
Mgombea wa udiwani kata ya nyasura kupitia chama cha mapinduzi CCM ndugu Magigi Samwel Kiboko amewaomba wanachama wa chama hicho kuwa watulivu na kuepuka vurugu katika kipindi chote kuelekea uchaguzi mkuu 2025.
Magigi ameyasema hayo leo tarehe 19 Aug 2025 baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo kwa msimamizi msaidizi watume huru ya taifa ya uchaguzi kwa kata ya Nyasura.

Wakati huo huo mgombea wa chama hicho cha mapinduzi kwa kata ya Kabarimu ndugu Ramadhan Kulwa Ngata amewataka wanachama wote wa CCM kuwa na umoja na mshikamano kuelekea uchaguzi mkuu huku akisisitiza kuwa umoja wao ndiyo ushindi.
Ngata pia ameyasema hayo mbele ya ofisi ya msimamizi msaidizi wa tume huru ya taifa ya uchaguzi kwa kata ya kabarimu baada ya kuchukua fomu ya kuwania udiwani wa kata hiyo kupitia CCM,