Mazingira FM

31 wajeruhiwa kwa mafuriko Musoma Mjini

19 August 2025, 9:54 am

JKikosi cha zimamoto na uokoaji Mara kikiendelea na juhudi za uokozi

Jitihada za kuokoa zinaendelea huku Majeruhi katika maafa haya ni watu 31 ikiwe watu wazima ni 11 na watoto wadogo 20.

Na Gabon Mariba – Musoma

Wakazi mbalimbali wa Manispaa ya Musoma Mkoani Mara wamejeruhiwa kutokana na Mafuriko ya Maji kufuatia Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani humo huku baadhi ya familia kukosa Makazi.

Wakizungumza Wananchi wa mtaa wa Machinjioni wanaomba kuboreshewa miundombunu, Hasa Karavati na Madaraja kupanuliwa ili kuweza kupitisha maji kwa wingi pindi Mvua zinapoongezeka hasa wakati wa Masika.

Sauti za baadhi ya wakazi wa manispaa ya Musoma walioathirika na mafuriko
Kamanda wa jeshi la Zimamoto na Uokozi Mkoa wa Mara Agastine Magere

Aidha Kamanda wa jeshi la Zimamoto na Uokozi Mkoa wa Mara Agastine Magere anaeleza mpaka sasa jitihada za kuokoa zinaendelea huku Majeruhi katika maafa haya ni watu 31 ikiwe watu wazima ni 11 na watoto wadogo 20.

Sauti ya Kamanda wa jeshi la Zimamoto na Uokozi Mkoa wa Mara Agastine Magere

Nae Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe.Juma Chikoka baada ya kufika eneo la tukio anatoa pole na kuahidi kusimamia baadhi ya changamoto katika kipindi hiki na kuhakikisha wananchi wanaendelea na majukumu yao ya kila siku.

Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Musoma walioathirika na mafuriko

Pia Chikoka akatoa rai kwa wananchi ambao baadhi yao wanatupa Taka hovyo katika miundombinu ya Maji na Madaraja jambo ambalo linapelekea kuziba mapitio ya maji pindi Mvua zinaponyesha.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe.Juma Chikoka