Mazingira FM
Mazingira FM
18 August 2025, 5:45 pm

Ni mgombea wa cha Democratic Party DP ambaye leo tarehe 18 Augost amechukua fomu za tume huru ya taifa ya uchaguzi ngazi ya jimbo akitaka kugombea ubunge na ngazi ya kata akitaka kugombea udiwani.
Na Adelinus Banenwa
Abubakari Makene Johnson amechukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge jimbo la bunda mjini kupitia chama cha Democratic Party DP.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Bunda mjini makene amesema ameamua kuchukua fomu kwa sababu anazo sifa za kugombea lakini pia matatizo ni mengi kwa jimbo la Bunda mjini ambapo anatamani akiwa mbunge aweze kuyashughulikia.

Makene ameongeza kuwa kwa muda mrefu wananchi wa jimbo la Bunda mjini wamepokea ahadi nyingi lakini zimekuwa ahadi ambazo hazitekelezeki ambapo wananchi wanyonge wamekata tamaa hivyo chama cha DP kikipewa ridhaa kitafanya mabadiriko makubwa kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.
Wakati huo huo katika hali ya isiyoyakawaida Abubakari Makene pia alipiga hodi kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Kabarimu kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya udiwani kwa kata ya Kabarimu.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu ya kugombea nafasi hiyo Makene amesema ni kweli ameamua pia Kugombea nafasi hiyo lengo likiwa ni kutaka kuleta maendeleo ambayo kwa muda mrefu wakazi wa Kabarimu wanatamani kuyafikia.
Amesema changamoto kubwa ni suala la miundombinu ya barabara na huduma za afya na endapo akichaguliwa na wananchi hicho kitakuwa kipaumbele chake.