Mazingira FM

Miradi ya zaidi ya bilion 3.5 kuzinduliwa na mwenge Bunda TC

13 August 2025, 7:28 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Aswege Enock Kaminyoge

Mapokezi ya mwenge huo ni shule ya msingi Balili Augost 15 2025 Asubuhi.

Na Adelinus Banenwa

Jumla ya miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi  bilioni 3.5 inatarajiwa kutembelewa na mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2025 kwa halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara.

Hayo ni kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Aswege Enock Kaminyoge.

Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake leo tarehe 13 Aug 2025  kuhusu mapokezi ya mbio za mwenge kitaifa kwa mkoa wa Mara kwa mwaka  2025 Mhe Aswege amesema shughuli ya mapokezi ya mwenge huo itafanyika shule ya msingi Balili kutokea mkoani Simiyu siku ya Augost 15 2025 asubuhi.

Ambapo mkuu wa mkoa wa Simiyu atakabidhi mbio hizo kwa mkuu wa mkoa wa Mara na kisha mwenge huo utaanza kukimbizwa kwenye halmashauri ya mji wa Bunda katika miradi mbalimbali ikiwemo ,  ujenzi wa maabala shule ya sekondari Paul Jones, barabara ya maduka sita,  uzinduzi wa shule ya sekondari nyasura, uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa maji Wariku miongoni mwa miradi mingine.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Aswege Enock Kaminyoge

Aidha Mhe mkuu wa wilaya amewaomba wakazi wote wa mji wa Bunda na viunga vyake kujitokeza kwa wingi katika mapokezi na mkesha wa mwenge ambao utakesha katika viwanja vya shule ya msingi Miembeni huku akisema kutakuwepo na shughuli nyingi zitakazofanyika ikiwemo kongamano la vijana na upimaji wa damu huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni ”jitokezeni kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu”

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Aswege Enock Kaminyoge