Mazingira FM

Mwenge wa uhuru kukimbizwa KM 152 Musoma

13 August 2025, 7:20 pm

Mkuu wa wilaya ya Musoma Mhe Juma Chikoka

Kwa wilaya ya Musoma mapokezi ni tarehe 16 katika kijiji cha Kabulabula halmashauri ya wilaya ya Musoma.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Musoma Mhe Juma Chikoka ameomba wakazi wote wa wilaya ya Musoma kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya mbio za mwenge kitaifa kwa wilaya ya Musoma ambapo amapokezi hayo kwa wilaya ya Musoma ni tarehe 16 katika kijiji cha Kabulabula halmashauri ya wilaya ya Musoma huku mkesha wa mwenge huo ukiwa katika viwanja vya shule ya msingi Bwai.

Mkuu wa wilaya ya Musoma Mhe Juma Chikoka

Akizungumza leo Tarehe 13 Aug 2025 kupitia radio mazingira fm kwenye  kipindi cha Asubuhi leo Mhe Chikoka amesema miradi mbalimbali inatarajiwa kutembelewa , kuzinduliwa na mingine kuwekewa mawe ya msingi ambapo mwenge huo utakimbizwa jumla ya kilometa 152 kwa siku mbili katika wilaya ya Musoma yenye halmashauri mbili za Musoma manispaa na Musoma DC.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Musoma Mhe Juma Chikoka