Mazingira FM
Mazingira FM
7 August 2025, 11:57 am

Kangi Lugola ampiku Kajege kura za maoni Mwibara huku Boni Getere aking’ara jimbo la Bunda
Na Adelinus Banenwa
Ni waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa zamani Kangi Lugola ameongoza kura za maoni za chama cha mapinduzi kwa jimbo la Mwibara akiwaacha watia nia wengine akiwemo mbunge aliyemaliza muda wake Charles Kajege.
Akitangaza matokeo ya kura hizo za maoni zilizopigwa Augost 4,2025 Mkurugenzi wa uchaguzi CCM wilaya ya Bunda Michael Chonya amesema watia nia kwa jimbo Mwibara walikuwa watia nia 6 huku Kangi Alphaxard Lugola akiongoza kwa kupata kura 2317 akiwapiku wengine akiwemo mbunge aliyemaliza muda wake Charles Muguta Kajege aliyepata kura 2091.

Wengine ni Wilson Mukama aliyepata kura 1017, Emmanuel Makale Busanya 168, Mbuta makanyaga 143 pamoja na Iddy Yazidi Mabara 42.
Wakati huohuo Michael Chonya amemtangaza Boniphas Mwita Getere kuongoza kwa kura 2119 kati ya kura 5332 halali zilizopigwa na wajumbe katika jimbo la Bunda.
Mwita Getere mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo la Bunda ameongoza mbele ya Aloyce Msafiri Msika aliyepata kura 1650, Lazaro William Kandole 1078, Daud Lukiko 411, Mosses Wambura Ryakitimbo 41 na ndugu Sulus Nyikera 33
Akizungumza Mara baada ya kutangazwa matokeo hayo Boniphase Getere ametoa shukrani kwa wajumbe wote waliomuamini huku akisema mchakato unaofuata ni vikao vya uteuzi ambavyo vinawajibu wa mwisho.