Mazingira FM
Mazingira FM
25 July 2025, 4:23 pm

Mambo ya kuzingatia kama kufanya maandalizi wakati wa kwenda kuripoti kwa kuhakikisha usalama wako kimazingira na hata kwenye mavazi.
Na Catherine Msafiri
Waandishi wa habari kutoka radio za kijamii wameaswa kuhakikisha wanakua na maandalizi mazuri ya namna ya kuripoti habari kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025
Hayo yamebainishwa na Nuzulack Dausen Afisa Mtendaji Mkuu, Nukta Africa wakati akitoa somo kuhusu namna mwanahabari anavyopaswa kuvizingatia kwenye kuripoti habari hususani za uchaguzi, mafunzo yaliofanyika mkoani Morogoro kwa siku tatu huku akiwasisitizia waandishi wa habari kuwa usalama wao ndio muhimu kuliko chochote.

Ndugu Dausen miongoni mwa mambo aliyobainisha ni kuhusu mambo ya kuzingatia kama kufanya maandalizi wakati wa kwenda kuripoti kwa kuhakikisha usalama wako kimazingira na hata kwenye mavazi.
Waandishi wa habari na wahariri waliohudhuria mafunzo hayo wamebainisha namna mafunzo waliopata yalivyo wajenga na kuwaandaa kueleza uchaguzi mkuu.
Nukta Africa imeandaa mafunzo ya jinsi ya kuthibitisha habari na kukabiliana na habari za uzushi/uongo kwa waandishi wa habari kutoka radio za kijamii na mkoani ambao ni wanachama hai wa Taasisi ya Maendeleo ya Vyombo vya Habari vya Kijamii (TADIO), yaliofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 23-25 july 2025 mkoani Morogoro.
Nukta Africa imetoa mafunzo hayo ya siku tatu (Julai 23-25, 2025) kwa kushirikiana na Shirika la International Media Support (IMS) na kwa msaada kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uswidi (SIDA).