Mazingira FM

Waandishi wanolewa kukabiliana na taarifa za uongo

25 July 2025, 4:09 pm

Waandishi wa habari na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari katika afunzo

Mafunzo haya yamelenga kuwajengea uwezo wanahabari nchini kufahamu mbinu za kugundua na kukabiliana na habari za uzushi kwa kutumia teknoloji.

Na Catherine Msafiri

Nukta Africa imeandaa mafunzo ya jinsi ya kuthibitisha habari na kukabiliana na habari za uzushi/uongo kwa waandishi wa habari kutoka radio za kijamii na mkoani ambao ni wanachama hai wa  Taasisi ya Maendeleo ya Vyombo vya Habari vya Kijamii (TADIO), yaliofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 23-25 july 2025 mkoani Morogoro

Mafunzo haya yamelenga kuwajengea uwezo wanahabari nchini kufahamu mbinu za kugundua na kukabiliana na habari za uzushi kwa kutumia teknolojia rafiki hasa wakati wa uchaguzi.

Akizungumza na radio Mazingira fm nje ya ukumbi wa mafunzo Daniel Samson Mkuu wa Mafunzo na Utafiti, Nukta Africa amesema kutokana na ongezeko la habari za uzushi na uongo mtandaoni hasa wakati huu kuelekea uchaguzi mafunzo haya yatawasaidia waandishi wa habari kudhibitisha taarifa za uzushi

Sauti ya Daniel Samson Mkuu wa Mafunzo na Utafiti, Nukta Africa
Waandishi wa habari na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari katika afunzo

Aidha amewaasa wanahabari na wananchi kuwa makini na kugundua taarifa za uzushi/uongo mtandaoni

Sauti ya Daniel Samson Mkuu wa Mafunzo na Utafiti, Nukta Africa

Kwa upande wao waandishi wa habari na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliopata mafunzo hayo wameeleza namna ambavyo mafunzo hayo yatakwenda kuwasadia kuzitambua habari za uzushi/uongo mtandaoni

Sauti za waandishi wa habari na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari

Nukta Africa imetoa mafunzo hayo ya siku tatu (Julai 23-25, 2025) kwa kushirikiana na Shirika la International Media Support (IMS) na kwa msaada kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uswidi (SIDA).