Mazingira FM
Mazingira FM
22 July 2025, 8:18 pm

Tukio la mama huyo kujinyonga limeacha maswali mengi kutokana na mume wake miaka miwili iliyopita alifariki kwa kujinyonga pia
Na Adelinus Banenwa
Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Pili Chacha (40) amefariki dunia kwa kujinyonga kwenye mti ulipo pembezoni mwa nyumba yake mtaa wa Migungani Bunda mjini

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema majira ya saa tano asubuhi walisikia kilio kutokea kwenye nyumba ya mama huyo na walipofika walikuta ni binti yake analia huku na kionesha kwenye kichaka pembeni mwa nyumba ambapo mama huyo alikuwa ameninginia.
Kwa upande wake Raitony Aloyce ambaye ni shemeji wa marehemu ameiambia mazingira fm kuwa tukio la shemeji yake kujinyonga limewauzunisha ambapo amesema marehemu ameacha watoto sita huku akisema hadi sasa familia haijui nini chanzo cha mama huyo kuchukua maamuzi hayo.
Mwenyekiti wa mtaa wa Migungani kata ya Bunda stoo halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara Jafeth Ryoba Marco amesema ni kweli tukio hiyo limetokea leo na baada ya kupewa taarifa na mtendaji aliwajulisha polisi waliofika eneo la tukio na kufanya vipimo kisha kukabidhi mwili kwa ndugu kwa ajili ya kuendelea na shughuli za mazishi .

Jafeth amesema tukio la mama huyo kujinyonga limeacha maswali mengi kutokana na mume wake miaka miwili iliyopita alifariki kwa kujinyonga pia hivyo kama wanamtaa na viongozi wamebaki na maswali