Mazingira FM
Mazingira FM
22 July 2025, 5:14 pm

uchaguzi huu umefanyika kwa mujibu wa ratiba na tayari kwa upande wa Bunda jumla ya madiwani viti maalumu 11 wamepatikana
Na Adelinus Banenwa
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Bunda Bi Marysiana Sabuni amesema mchakato wa kura za kuwapata madiwani viti maalumu kwa tarafa nne za wilaya ya Bunda umeenda vizuri bila changamoto.
Akizungumza na Mazingira Fm ofisini kwake Bi Marysiana amesema uchaguzi huu umefanyika kwa mujibu wa ratiba na tayari kwa upande wa Bunda jumla ya madiwani viti maalumu 11 wamepatikana ikiwa ni pamoja na watano kwa Halamshauri ya mji wa Bunda na sita kwa Halmashauri ya wilaya ya Bunda.
Aidha Bi Marysiana amewataka wanajumuiya wote wa UWT kuwa kitu kimoja baada ya uchaguzi huo na kinachosubiriwa sasa ni uteuzi wa majina ya madiwani ambao watapeperusha bendera za chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025