Mazingira FM
Mazingira FM
9 July 2025, 11:23 am

Tukio hilo limetokea wakati mtoto huyo akivuka barabara akitoka shuleni,
Na Adelinus Banenwa
Mtoto mwenye umri wa miaka 8, Joseph Masinde, mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Kabarimu B, amefariki dunia leo baada ya kugongwa na pikipiki maarufu kama bodaboda katika barabara ya Mwanza–Musoma, eneo la Bunda.
Tukio hilo limetokea wakati mtoto huyo akivuka barabara akitoka shuleni, baadhi ya mashuhuda wameelezea tukio hilo
Masinde Magoti ni Baba mzazi wa mtoto huyo, amesema alipokea taarifa za ajali hiyo akiwa kazini na alipoenda Hospitali ya DDH Bunda, alikuta mtoto wake tayari amefariki dunia.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mapinduzi, kata ya Bunda Mjini, Daniel Yapanda, amethibitisha kutokea kuwa eneo hilo limekuwa likishuhudia matukio ya ajali mara kwa mara, hasa wakati wa watoto kuvuka barabara wakitoka au kuelekea shule, na ametoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua madhubuti ili kuzuia ajali kama hizi siku zijazo.
jitihada za kuwatafuta jeshi la polisi zindaendelea
Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitalini huku taratibu za mazishi zikiendelea.