Mazingira FM
Mazingira FM
3 July 2025, 7:27 pm

Kwa mujibu wa Chonya idadi hiyo inaonesha mwitikio mkubwa wa wanachama wa CCM kushiriki katika mchakato wa kisiasa, hali inayoakisi ukuaji wa demokrasia ndani ya chama.
Na Adelinus Banenwa
Jumla ya wagombea 42 wametia nia ya kuomba kuteuliwa kwenyenafasi ya ubunge Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Wilaya ya Bunda.
Kati ya hao, wagombea 15 wanawania ubunge katika Jimbo la Mwibara, wagombea 14 katika Jimbo la Bunda Mjini, na wagombea 13 katika Jimbo la Bunda.
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu wa CCM Wilaya ya Bunda, Michael Chonya, alipokuwa akizungumza na Redio Mazingira FM mapema leo.
Michael Chonya amesema idadi hiyo inaonesha mwitikio mkubwa wa wanachama wa CCM kushiriki katika mchakato wa kisiasa, hali inayoakisi ukuaji wa demokrasia ndani ya chama.
Chonya amesema Kwa sasa, chama hicho kinaendelea na hatua za awali za uchambuzi wa fomu na majina ya wagombea, huku akibainisha kuwa mchakato wa vikao unaanza rasmi july 4 kwa ngazi ya kata kupiamajina ya watia nia kwa ngazi ya udiwani
Aidha, amewataka wanachama wote na wagombea kuwa watulivu wakati wote wa mchakato wa kura za maonihuku akiwahakikishia kuwa haki na usawa vinazingatiwa.