Mazingira FM

Changamoto za kijinsia na kitamaduni kuelekea Uchaguzi Mkuu Tanzania 2025

3 July 2025, 10:09 am

Mfano wa sanduku la kura

Je, vyama vya siasa vina nafasi gani katika kuvunja vizingiti hivi?

Na Edward Lucas na Dinnah Shambe

Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania Oktoba 2025, makala hii maalum ya redio inachambua kwa undani sababu zinazowafanya wanawake wengi kuogopa au kushindwa kushiriki kikamilifu katika siasa, hasa kwa kuwania nafasi za uongozi. Je, mila na desturi kandamizi bado ni kikwazo? Je, vyama vya siasa vina nafasi gani katika kuvunja vizingiti hivi?

Katika makala hii tutawasikiliza wanawake waliowahi kugombea nafasi za uongozi, viongozi wa kisiasa, taasisi ya TAMWA, pamoja na wananchi wa kawaida tukipata simulizi halisi, changamoto walizopitia, na matumaini ya mabadiliko.

Makala yanayoangazia changamoto za kijinsia na kitamaduni kuelekea Uchaguzi Mkuu Tanzania 2025