Mazingira FM
Mazingira FM
29 May 2025, 7:54 pm

Kwa mujibu wa muongozo uliopo wakulima wote wa zao la pamba wamesamehewa madeni ya mkopo wa pembejeo.
Na Adelinus Banenwa
Katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Mtelela amewaagiza AMCOS kujiepusha na udanganyifu wa kilo za pamba kwa lengo la kukwepa ushuru unaotakiwa kulipwa .
Mtelela ameyasema hayo katika kikao cha wadau wa zao la pamba wilayani Bunda kilichoketi kwa lengo la kuwapatia AMCOS mikataba pamoja na maelekezo kuelekea ufunguzi wa ununuzi wa zao la pamba wilayani Bunda
Kwa upande wake mkaguzi wa zao la pamba wilayani Bunda ndugu Hemedi Kabea amesema kwa mujibu wa muongozo uliopo wakulima wote wa zao la pamba wamesamehewa madeni ya mkopo wa pembejeo, hivyo ni marufuku kwa kiongozi wa AMCOS yeyote kumkata mkulima fedha ya mkopo wa pembejeo.

Naye meneja wa bodi ya pamba mkoa wa Mara Baraka Kiboye amesema kampuni itakayokuwa inapandisha bei ya pamba hiyo ndiyo itakayokuwa inanunuliwa pamba kwenye AMCOS .
Pia ameongeza kuwa inapotokea kuna mabadiliko ya bei viongozi wa AMCOS wanatakiwa kusaini ili kuepuka mkono wa sheria kwa kujaribu kwaibia wakulima.