Mazingira FM
Mazingira FM
24 May 2025, 8:41 pm

Ni jukumu la vijana hao kuhakikisha wanwalinda viongozi pia wanajitokeza kugombea nafasi za uongozi pindi mchakato wa chama utakapoanza
Na Adelinus Banenwa
Katibu wa jumuiya ya umoja wa vijana chama cha mapinduzi wilaya ya Bunda Pendo Machilu amewataka vijana kuacha woga na kujitokeza kugombea nafasi za uongozi kwa udiwani na ubunge katika uchaguzi mkuu wa 2025.
Pendo ameyasema hayo leo May 24 2025 wakati akizungumza kwenye baraza la umoja wa vijana CCM kata ya nyamakokoto ambapo amesema ni jukumu la vijana hao kuhakikisha wanwalinda viongozi pia wanajitokeza kugombea nafasi za uongozi pindi mchakato wa chama utakapoanza.
Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja huo kwa kata ya Nyamakokoto ndugu Anthony Dickson amesema ujumbe alioutoa katibu wa jumuiya hiyo wilaya ya Bunda umekuwa chachu kwa vijana waliokuwa na mashaka juu ya kugombea nafasi za uongozi
Aidha ndugu Anthony Dickson amewahimiza vijana wote kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura ili wawachague viongozi watakaowaletea maendeleo katika maeneo yao.